Friday, October 30, 2009

Climate change in Kilimanjaro

MABADILIKO YA HALI YA HEWA MLIMA KILIMANJARO

Mabadiliko ya Tabia ya nchi ama mabadiliko ya hali ya hewa ni suala ambalo hivi sasa linaikabili Dunia nzima .
.
Mabadiliko haya ya hali ya hewa yanaonekana kuathiri zaidi nchi zilizo katika Bara la Afrika ,Hali hii ya mabadliko ya hali ya hewa inakusudiwa kuathiri ama kuhatarisha juhudi za maendeleo katika nchi mbalimbali.

Suala hili la mabadiliko ya tabia ya Nchi limeanza kuonekana katika Mlima Kilimanjaro Nchini Tanzania , Ambako theruji iliyokuwa kivutio kikubwa kwa watalii inayeyuka kwa kasi na inazidi kuyeyuka kadri siku zinavyokwenda na pengine huenda ikaisha kabisa

Zipo sababu nyingi zinazoelezwa kusababisha kuwepo kwa mabadiliko ya hali ya hewa katika mlima kilimanjaro sababu ambazo zinasababishwa na utumiaji wa nishati za carbon gas emissions pia Umwagaji wa hewa chafu umechangia kuharibu mazingira katika mlima huo hali inayo sababisha ongezeko kubwa la joto

Mabadiliko ya hali ya Hewa katika mlima Kilimanjaro unasabishwa pia na wakazi wa maeneo hayo kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya uhifadhi wa mazingira hali inayopelekea kukata miti ovyo, kuchoma mikaa katika mazingira haya ya mlima , na mambo mengine mengi ambayo wakazi wanayafanya bila wao kujua kwamba wanaharibu na kusababisha madhara yatokanayo na mabadiliko ya hali ya hewa.

Hali ya hewa katika mlima Kilimanjaro awali ilikuwa ni ya ubaridi lakini kutokana na barafu kuyeyuka na nyuzi joto kuongezeka mazingira katika mlima huu yanabadilika pia na makazi ya watu yanaonekana kutofaa hususani kwa wakazi wa Bondeni wanaotegemea maji yanayotiririka toka mlimani kwa ajili ya shughuli mbalimbalihuenda wakajikuwa wamekuwa wakimbizi wa mazingira .


Hata hivyo suala hili la uchafuzi wa mazingira limeonekana kusababishwa zaidi na watu wa nchi anbazo zimeendelea,Nchi hizi zimeonekana kuharibu na kuchafua mazingira kuliko watu wote.Na matokeo yake ni kwamba waathirika ni Nchi zinazoendelea. kinachositikisha ni kwamba wale wanao haribu wanaonekana kutoathirika sana kwa vile tayari wamekwisha jiandaa kwa kujiwekea, makazi ambayo, yanaweza yakastahamili zaidi, wana nyumba madhubuti ambazo haziangushwi kwa upepo huu wa kawaida. , kwa mfano, nchi. kama Japan sasa hivi tetemeko la ardhi sio tishio kwa nchi hiyo; kwa sababu yale majengo yamejengwa kitaalamu. Yanastahamili na pia nchi hizi zimeimarisha kila aina ya miundombinu.

Mabadiliko ya hali ya hewa katika mlima Kilimanjaro yanazidi kuleta changamoto nyingi zikiwemo, kupungua kwa watalii ambao walikuwa wakija kutazama theruji, kilimo kimekuwa cha kusuasua kwani sasa hivi migomba haipati maji ya kutosha. Suala hili la mabadiliko ya hali ya hewa linahitaji ushirikiano wa mataifa kwa vile ni suala ambalo linahitaji ushirikiano kati ya nchi zilizoendelea na zile zinazoendelea.

No comments:

Post a Comment